Maafisa wa umma wanaotaka kugombea 2027 kujiuzulu kufikia Februari 9

Martin Mwanje
1 Min Read
Maafisa wa IEBC wakati wa uzinduzi wa Mpango wa Kimkakati wa mwaka 2024–2029 na Mpango wa Kusimamia Uchaguzi wa mwaka 2025-2027

Maafisa wote wa umma wanaopanga kugombea nyadhifa mbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 wametakiwa kujiuzulu kufikia Februari 9 mwaka ujao. 

Hayo yamebainika wakati wa hafla ya uzinduzi wa Mpango wa Kimkakati wa IEBC wa mwaka 2024–2029 na Mpango wa Kusimamia Uchaguzi wa mwaka 2025-2027 iliyofanyika jijini Nairobi leo Jumatano.

Kwa mujibu wa IEBC, kampeni rasmi ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 itaanza Mei 29 na kumalizika Agosti 7, 2027 siku tatu kabla ya kuandaliwa kwa uchaguzi mkuu.

Kampeni hizo zitafanyika kati ya saa moja asubuhi na saa kumi na mbili jioni.

Shughuli ya kuwasajili wapiga kura nayo itafungwa Juni 12 mwakani, kwa mujibu wa ratiba ya IEBC.

Uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 utaandaliwa Agosti 10 na tayari wanasiasa wameanza kufanya kampeni hata kabla ya kipenga rasmi cha kufanya hivyo kupulizwa.

Share This Article