Waakilishi wa Afrika katika fainali za mwaka huu za Kombe la Dunia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, walisalimu amri na kupigwa bao moja kwa bila na Colombia mapema Jumatano katika uwanja wa Guadalajara, nchini Mexico.
Bao la ushindi kwa Colombia lilipachikwa kimiani katika dakika ya 76 na Daniel Munoz ,matokeo yanayowafuzisha Colombia kwa awamu ya 32 bora,wakiwa na alama 6 kileleni pa kundi K,alama 2 zaidi ya Ureno iliyowakomoa limbukeni Uzbekistan mabao 5-,0 katika mechi ya Jumanne.
Timu saba zimefuzu kwa raundi ya 32 bora baada ya kumalizika kwa mechi za mzunguko wa pili hatua ya makundi zikiwa,mabingwa watetezi Argentina,Colombia,waandalizi wenza Mexico na Marekani,Ujerumani,Ufaransa na Norway.
Mechi za mwisho hatua ya makundi zitaanza Jumatano kwa jumla ya mechi sita za makundi ya A,B na C kati ya leo usiku na mapema kesho.