Kampuni ya magari ya kuagiza mitandaoni ya Little Cab kwa ushirikiano na Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru nchini (KRA), imezindua matumizi ya risiti za eTIMS kwa wateja wa mashirika wanaosafiria magari hayo.
Ushirikiano huo ni sehemu ya mpango wa uhamasishaji kwa wafanyabiasahara nchini kuhusu umuhimu wa kutumia eTims.
Akizungumza wakati wa kusaini ushirikiano huo, Naibu Kamishna wa KRA anayehusika na eTIMS Caroline Wacuka alipongeza ushirikiano huo akisema utaleta uwajibikaji wa ushuru.
Mpango huo maarufu kama “Every Ride, Invoiced & Tax Compliant,” unalenga kuwahamasisha madereva, wafanyaboashara, abiria na wasafiri kuhusu umuhimu wa kutumia mfumo wa eTIMS katika utoaji risiti za KRA.

Meneja wa mahusiano katika kampuni ya Little Cab Nyawira Maina amesema mfumo huo mpya utawasaidia wasafiri wa kutoka kwa mashirika kutumia teknoljia ya kisasa ya utoaji risiti.