Wafanyakazi wawili wa Mamlaka ya Bandari nchini, KPA wameshtakiwa pamoja na wenzao ambao hawakuwa mahakamani kwa ulaghai.
Wafanyakazi hao wanadaiwa kutoa shilingi milioni moja kutoka kwa akaunti ya Chama cha Wafanyakazi wa Bandarini iliyoko kwenye chama cha akiba na mikopo cha Bandari DT SACCO bila ruhusa.
Kibibi Omery na Mejuma Chirau walifikishwa mbele ya Hakimu Mkuu Eric Wambo katika mahakama ya Mombasa na kukanusha mashtaka.
Waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi 500,000 na mdhamini wa kiasi kama hicho au dhamana ya shilingi 200,000 pesa taslimu.
Kesi hiyo itatajwa Oktoba 12, 2026.
Taarifa ya Sadiq Hassan wa KNA