Oburu Oginga yuko nchini Uingereza kwa uchunguzi wa kimatibabu

Tom Mathinji
1 Min Read
Dkt. Oburu Oginga - Kinara wa ODM

Kiongozi wa chama cha Orange Democtratic Movement (ODM) Oburu Oginga yuko nchini Uingereza kwa uchunguzi wa kimatibabu.

Kupitia kwa taarifa, Oginga alisema ziara hiyo ya itamwezesha kufanyiwa uchunguzi kamili wa kimatibabu, huku akitumia muda huo kupumzika kufuatia ushauri wa madaktari wake.

Aidha, Oginga alielezea imani na muundo wa chama cha ODM, kutekeleza shughuli za kila siku bila kutatizwa.

“Huu ni wakati wa mabadiliko, ambapo chama cha ODM kinapitia majaribu kuhusu utayari wa kitaasisi,” alisema Oburu.

Akiwa katika ziara hiyo ya matibabu, shughuli za chama cha ODM zitaongozwa na Manaibu wa chama hicho Simba Arati na Abdulswamad Shariff Nassir, pamoja na Kamati ya Kitaifa ya chama hicho.

“Kama mzee aliyetembea safari hii ndefu pamoja nanyi, nina imani na uongozi wao, nidhamu na maono wa kuongoza chama hiki kikamilifu,” alidokeza Oginga.

Aliwahimiza wanachama wa ODM na maafisa kushirikiana na uongozi wa chama, kudumisha umoja na kuangazia malengo ya kitaifa ya chama hicho.

Share This Article