Ugomvi wa kifamilia wasababisha maafa Trans Nzoia

DCI ilisema kuwa Wamuloli alitoroka baada ya kisa hicho, hatua iliyosababisha maafisa wa polisi kuanzisha msako dhidi yake.

Tom Mathinji
1 Min Read
Ugomvi wa kifamilia wasababisha maafa Trans Nzoia.

Maafisa wa usalama wanamzuiliwa mshukiwa anayedaiwa kumuua kaka yake baada ya ugomvi kati yao, katika kaunti ya Trans Nzoia.

Kulingana na Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Nelson Wanundu alizozana na kaka yake Isaak Walumoli baada ya kutofautiana, ambapo Wanundu alijeruhiwa vibaya na kupelekwa hospitalini kwa matibabu lakini akatangazwa kuwa amefariki.

DCI ilisema kuwa Wamuloli alitoroka baada ya kisa hicho, hatua iliyosababisha maafisa wa polisi kuanzisha msako dhidi yake.

“Baada ya kupokea habari za kijasusi, maafisa wa polisi walimkamata mshukiwa huyo Kitale mjini na anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Kiminini akisubiri kufunguliwa mashtaka,” ilisema DCI.

Mwili wa marehemu unahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya  Kiminini, ukisubiri kufanyiwa upasuaji.

DCI  imeelezea kujitolea kwake kukamilisha uchunguzi na kuhakikisha haki inapatikana.

Share This Article