Watu wawili wamethibitishwa kufariki baada ya dereva wa lori lililokuwa likisafirisha saruji kuelekea Marimanti kupoteza mwelekeo na lori hilo kubingiria katika mto Thingithu.
Mto huo unapatikana kwenye barabara ya Chiakariga- Marimanti katika eneo bunge la Tharaka, kaunti Tharaka Nithi.
Kulingana na polisi, watu wengine wawili waliokuwa kwenye lori hilo walinusurika ajali hiyo na kwa sasa wanapokea matibabu katika hospitali ya Marimanti Level 4.
Akithibitisha ajali hiyo, OCPD wa Tharaka Kusini Christopher Nyamai alisema lori hilo lilikuwa likitoka Chiakariga kuelekea Marimanti wakati dereva alipopoteza mwelekeo na kubingiria mtoni.
Taarifa ya Njeru Kiara