Viongozi wa Tanzania na Rwanda, wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa nchini hizo mbili ili kukuza utangamano wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Rais Paul Kagame wa Rwanda na Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, waliafikiana haya walipokutana jijini Dar es Salaam,Tanzania Jumapili jioni.
Viongozi hao wawili walisema ushirikiano huo wa Rwanda na Tanzania, utakuwa wenye manufaa makubwa kwa nchi hizo mbili na Jumuia ya EAC.
Rais Samia alihimiza haja ya kuongeza kasi ya kuondoa vikwazo ili kukuza soko la pamoja kwa nchi za Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.
Rais Kagame alikuwa Tanzania kwa ziara rasmi ya siku moja.