Makala ya 23 ya fainali za Kombe la Dunia yataingia siku ya 22 leo Alhamisi kwa jumla ya michuano mitatu ya awamu ya 32 bora.
Timu 10 tayari zimefuzu kwa hatua ya 16 bora kufikia sasa, zikiwemo wenyeji Mexico, Marekani na Canada.
Mataifa mengine yaliyofanikiwa kuingia raundi ya 16 ni Ufaransa, Morocco, Uingereza, Norway, Brazil, Paraguay na Ubelgiji.
Mechi za awamu ya 32 zitakamilika mapema Jumamosi kabla ya kupisha mzungo wa 16 bora kuanzia Jumamosi usiku.
Austria watakabiliana na Uhispania kaunzia saa mbili usiku uwanjani Los Angeles kabla ya kuwapisha Ureno na Croatia, watakaopimana nguvu saa nane usiku katika uwanja wa Toronto, nao Algeria wahitImishe ratiba mapema saa kumi na mbili asubuhi Ijumaa dhidi ya Uswizi mjini Vancouver.