Mabingwa watetezi wa Kombe la Ligi ya Afrika BAL Petro de Luanda ya Angola, watachuana na Al Ahli Tripoli ya Libya, kwenye fainali ya mwaka 2025 mjini Pretoria, Afrika Kusini, Jumamosi hii.
Al Ahli Tripoli waliwapiku APR ya Rwanda alama 84-71 katika nusu fainali huku Petro, wakiimenyan Al Ittihad ya Misri, pointi 96-74 katika nusu fainali nyingine.
Al Ittihad watakabiliana na APR katika mchuano wa kuwania nishani ya shaba kesho Ijumaa.