Sekta ya Michezo yatengewa bajeti ya shilingi bilioni 16.69

Wizara ya michezo kwa jumla imetengewa shilingi bilioni 16.69.

Dismas Otuke
1 Min Read

Michezo ni mojawapo wa sekta zilizonufaika kwa kupata nyongeza ya mgao wa fedha kwenye makadario ya bajeti ya matumizi ya fedha mwaka 2025/2026, iliyosomwa bungeni leo na Waziri wa Fedha John Mbadi.

Wizara ya michezo kwa jumla imetengewa shilingi bilioni 16.69.

Kati ya kiwango hicho, shilingi milioni 241 zimetengewa shirika la kukabiliana na ulaji muku nchini ADAK, baada ya bajeti hiyo kukatwa katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.

Hii ni afueni huku Kenya ikiimarisha vita dhidi ya ulaji muku kuelekea kwa makala ya 20 ya mashindano ya Riadha Duniani mjini Tokyo,Japan,kati ya Septemba 13 na 21 mwaka huu.

Aidha, kiwango kingine kitatumika kwa maandalizi ya fainali za nane za Kombe la Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Nyumbani CHAN kati ya Agosti 2 na 30 mwaka huu.

Kenya itakuwa mwenyeji wa CHAN pamoja na Tanzania na Uganda.

Website |  + posts
Share This Article