Wizara ya Kilimo yapoteza shilingi bilioni saba kwenye bajeti ya 2025/2026

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Fedha John Mbadi.

Wizara ya Kilimo imepunguziwa mgao wake baada ya kutengewa shilingi bilioni 47.6 kwenye bajeti ya mwaka 2025/2026, ikilinganishwa na shilingi bilioni 54.6 ilizotengewa katika mwaka wa kifedha wa 2024/2025. 

Mgao katika wizara hiyo umepunguzwa licha ya kuwa sekta ya kilimo imechangia asilimia 22.5 kwa pato jumla la taifa hili na pia imechangia moja kwa moja kwa maisha ya mamilioni ya wakenya.

Aidha mgao huo wa sekta ya Kilimo, unahusisha takriban asilimia tatu pekee ya bajeti jumla  ya nchi hii.

Akiwasilisha ya bajeti ya mwaka 2025/26 kwenye majengo ya bunge leo Alhamisi, waziri wa Fedha John Mbadi alisema miongoni mwa walionuifaika zaidi kwenye mgao wa sekta ya kilimo, ni mradi wa kitaifa wa uongezaji thamani ya mazao ya kilimo-NAVCDP,  ambao utapokea shilingi bilioni 10.2.

Mpango wa mbolea ya gharama nafuu umedumisha kiwango cha shilingi bilioni nane, huku magauzi katika sekta ya sukari yakitengewa shilingi bilioni 1.5.

Wakati huo huo mradi wa uuzaji wa mifugo hapa nchini ulitengewa shilingi bilioni 1.6, huku ule wa uongezaji akiba ya chakula na uanuwai wa mimea ukipokea shilingi Bilioni 1.2.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article