Washukiwa wa ulanguzi wa mihadarati wakamatwa Nairobi

Tom Mathinji
1 Min Read
Mihadarati yapatikana kwenye karakana Ruaka, Nairobi.

Maafisa kutoka kitengo cha kukabiliana na Mihadarati (ANU) na wale wa kukabiliana na Uhalifu wa Kupangwa (TOCU), wamewakamata washukiwa wawili na kupata mihadarati kwenye karakana moja eneo la Ruaka, kaunti ya Nairobi.

Kupitia kwa taarifa, maafisa hao waliopokea habari za kijasusi, walifanya msako kwenye karakana hiyo eneo la Riverside na kupata mihadarati hiyo iliyokuwa imefungwa kwa mifuko ya samawati na kuwekwa kwenye sanduku la chuma.

Kupitia kwa ukurasa wa X, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), ilisema washukiwa wawili Nasiim Abdallah na Trevas Mungai Okoth, walikamatwa kwenye operesheni hiyo na wanazuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Muthaiga, wakisubiri kufikishwa mahakamani.

Maafisa hao walipata mifuko 12 iliyokuwa na bangi, mashini ya kupima uzani na vifaa kadhaa vya kupakia, ambavyo vinazuiliwa kama ushahidi kwenye kesi hiyo.

TAGGED:
Share This Article