Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa, ametoa wito kwa viongozi ndani ya serikali jumuishi kuweka kando mizozo na kuangazia kuwaunganisha wakenya.
Barasa alielezea wasiwasi kuhusu ongezeko la mizozo ndani ya serikali jumuishi, aliyosema yanadumaza maendeleo.
Alidokeza kuwa lengo kuu la serikali jumuishi ni kuleta Umoja wa kitaifa na kuchochea maendeleo kwa manufaa ya raia wa Kenya.
Gavana huyo alitoa wito kwa viongozi kudumisha moyo wa ushirikiano na demokrasia, akionya kuwa mizozo ya ndani ya muungano huo utasambaratisha utoaji huduma kwa wananchi.
Barasa aliyasema hayo siku ya Ijumaa katika uwanja wa Bukhungu wakati wa hafla ya utoaji wa ruzuku ya shilingi milioni 12 kwa vijana 3,000 wa mpango wa uwezeshaji wa vijana na wa awake katika kaunti hiyo.