Jitokezeni kwa wingi mpige kura, mgombea wa UDA awasihi wakazi wa Ol Kalou

Martin Mwanje
1 Min Read
Mgombea wa UDA Muchina Nyagah akiwahutubia wanahabari baada ya kupiga kura

Mgombea wa UDA katika uchaguzi mdogo wa Ol Kalou Samuel Muchina Nyagah ametoa wito kwa wakazi wa eneo bunge hilo kujitokeza kwa kwingi na kupiga kura zao kabla ya vituo kufungwa. 

“Natoa wito kwa wakazi wa Ol Kalou kujitokeza kwa wingi na kumchagua mbunge atakayewatumikia kwa kipindi cha mwaka mmoja ujao,” alisihi Nyagah.

“Najua nashinda, lakini niko tayari kukubali chochote ambacho watu wa Ol Kalou wataamua debeni.”

Wito wake unakuja huku wakazi wa Ol Kalou wakiendelea kupiga kura katika uchaguzi mdogo unaoandaliwa na Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) leo Alhamisi.

Kwa kawaida, chaguzi ndogo huwa hazivutii idadi kubwa ya wapiga kura.

Eneo bunge la Ol Kalou lina jumla ya wapiga kura 73, 480 na vituo 144 vya kupigia kura.

Vituo vya kupigia kura vinatarajiwa kufungwa majira ya saa kumi na moja jioni.

 

Share This Article