Waliokuwa karantini kuchunguzwa Ebola kuondoka Jumapili

Dkt. Amoth alitoa wito kwa Wakenya kuwapokea watu hao, akiongeza kuwa hawawezi kusababisha maambukizi ya ugonjwa huo kwa wengine.

Tom Mathinji
1 Min Read
Dr. Patrick Amoth - Mkurugenzi Mkuu wa Afya nchini Kenya.

Watu waliokuwa wakizuiliwa karantini kuchunguzwa ikiwa wameambukizwa ugonjwa wa Ebola, wataondoka siku ya Jumapili. Hayo ni kulingana na Mkurugenzi Mkuu wa Afya Dkt. Patrick Amoth.

Kulingana na Wizara ya Afya, watu hao wanaoshukiwa walitangamana na mwathiriwa wa kwanza kabisa wa ugonjwa huo hapa nchini, wataondoka karantini baada ya kukamilisha siku 21 bila kuonyesha dalili za ugonjwa huo.

Dkt. Amoth alitoa wito kwa Wakenya kuwapokea watu hao, akiongeza kuwa hawawezi kusababisha maambukizi ya ugonjwa huo kwa wengine.

Hayo yanajiri huku taifa hili likinakili vifo viwili kutokana na makali ya virusi hivyo, mwathiriwa wa hivi punde akiwa mwanamke mwenye umri wa miaka 65 na ambaye ni jamaa wa mwathiriwa wa kwanza. aliyeaga dunia usiku wa Ijumaa.

Wagonjwa wanane wanaendelea kupokea matibabu katika vituo tofauti vya afya vilivyotengwa, hali yao ya afya ikitajwa kuwa imara.

Wizara ya Afya imethibitisha kuwa wale wote waliotangamana na mgonjwa wa kwanza wamepatikana, huku idadi ya kesi zilizothibitishwa nchini ikisalia kuwa tisa.

Share This Article