Gavana wa Kaunti ya Kwale Fatuma Achani, amezindua ugavi wa miche ya matunda 33,000 ya miembe,michungwa, mikorosho na minazi kwa wakulima 5,000 wa Kaunti hiyo.
Kufikia sasa Serikali ya Kaunti ya Kwale imepeana miche ya matunda kwa wakulima zaidi ya 10,000 katika Kaunti hiyo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Achani alisema kuwa miche hiyo itagawanywa kwa wakulima hao ili kupiga jeki uzalishaji wa matunda katika kaunti hiyo na pia kuzalisha mali ghafi kwa kiwanda cha matunda kinachoendelea kujengwa katika eneo la Shimbahills.
Aidha, Achani alitoa wito kwa wakulima wa Kwale kufuata maagizo ya maafisaa wa Kilimo wakati wa upanzi wa miche hiyo, na kukumbatia Kilimo cha kisasa.