Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki amesema ni sharti bara Afrika linapswa kufadhili ajenda zake za amani, usalama na maendeleo kupitia ukusanyaji wa mapato, soko la mtaji, mifumo jumuishi ya malipo na taasisi za fedha.
Akizungumza siku ya Ijumaa wakati wa kongamano la 12 la Tana ambalo liliwaleta pamoja viongozi wa ngazi za juu serikali kujadili usalama barani Afrika Jijini Bahir nchini Ethiopia, Kindiki alisema bara hili ni lazima litumie rasilimali zake vyema pamoja na uwezo wake wa kiuchumi katika ushawishi mkubwa kuhusiana na maamuzi yanayoathiri wakazi wake.
Alitoa wito kwa mataifa ya Afrika kubuni taasisi thabiti za serikali ili kushughulikia mizozo, ugaidi na uhalifu wa kupangwa, akidokeza kuwa amani ya kudumu pamoja na uhuru ni masuala yanayotegemea uwezo wa serikali wa kudhibiti changamoto za kiusalama.
“Afrika lazima iwe na taasisi thabiti na utangamno wa kiuchumi,” alisema Kindiki.
Naibu huyo wa Rais alisema Afrika in madini, ardhi na idadi kubwa ya watu, lakini ina ushawishi mdogo wa maamuzi kuhusu maswala yanayowaathiri watu wake.