Matatu kuongeza nauli kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta

Karakacha ameongeza kuwa hawana budi kupandisha nauli kutokana na kuongezeka kwa gharama  za kila siku kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta.

Dismas Otuke
1 Min Read

Magari ya uchukuzi wa umma maarufu kama Matatu yametangaza kuwa yataongeza  nauli inayotozwa siku moja baada ya mamlaka ya kuthibiti kawi na bidhaa za Petroli (EPRA ) kuongeza bei ya mafuta.

EPRA iliongeza bei ya Petroli kwa shilingi 12 na senti 93 ,Dizeli ikaongezeka kwa shilingi 9 na senti  90,wakati mafuta taa yakipaa kwa shilingi 28 na senti 49 kwa kila lita moja.

Chama cha wamiliki wa Matatu nchini (MOA) kimeishutumu serikali kwa kukiuka makubaliano ya mwezi Mei mwaka huu na Rais William Ruto katika Ikulu ya Mombasa ndiposa wakasitisha mgomo wa kitaifa.

Mwenyekiti wa MOA Albert Karakacha, amesema hawana budi kuongeza nauli kwani bei ya Dizeli imepanda kwa shilingi 9 na senti 90, kinyume na makubaliano yao na Rais mwezi Mei ya kuzuia kupanda kwa bei ya bidhaa hiyo.

Karakacha ameongeza kuwa hawana budi kupandisha nauli kutokana na kuongezeka kwa gharama  za kila siku kufuatia kupanda kwa bei ya mafuta.

 

TAGGED:
Share This Article