Maafisa wa polisi wamenasa bidhaa zinazodaiwa kuwa za wizi kwenye operesheni iliyotekelezwa katika eneo la Marurui.
Bidhaa hizo zilipatikana baada ya kukamatwa na kuwasilishwa mahakamani kwa Haren Kumar Damji Mandavia, ambaye anakabiliwa na kesi ya kupata bidhaa kwa njia za ulaghai.
Baada ya kupokea habari za kijasusi, maafisa wa polisi walipata bidhaa za rangi zilizopatikana kwa njia za ulaghai katika eneo la Marurui kwenye barabara ya Northern Bypass.
Mmoja wa wenye bidhaa hizo alifanikiwa kutambua bidhaa zake alizowasilisha kwa mnunuzi huyo mlaghai.
Baadhi ya bidhaa zilizopatikana ni pamoja na mafuta za viwanda, betri za pikipiki na za injini za magari, vifaa vya taa aina ya LED, mapambo ya ukuta na zile za nyumbani.
Kupitia ukurasa X, Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), ilisema uchunguzi unaendelea kubainisha umiliki wa ghala hilo na uwezekano wa uhusiano wake na shughuli za uhalifu.
Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa mshukiwa aliyekamatwa na washirika wake ni sehenu ya sakata pana ya visa vya wizi wa bidhaa vilivyoripotiwq kote nchini.
Wananchi ambao huenda wamepoteza Mali yao wamehizwa kuripoti katika kituo cha polisi kilicho karibu.