Winnie Byanyima: Kizza Besigye amerejeshwa gerezani

Besigye,  amewahi kugombea urais wa Uganda mara nne bila mafanikio.

Tom Mathinji
1 Min Read
Dkt. Kizza Besigye - Kiongozi wa upinzani nchini Uganda

Winnie Byanyima ambaye ni mke wa Kizza Besigye, amesema kuwa kiongozi huyo wa upinzani amerejeshwa gerezani licha ya afya kudhoofika.

Besigye alikuwa amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Rufaa ya Mulago baada ya kuzirai akihudhuria kikao cha mahakama 29 Julia, 2026.

Kupitia ukurasa wa X, Winnie alisikitika kuwa maafisa wa magereza walimrejesha gerezani Besigye, akiwa mgonjwa na angali mnyonge.

“Baada ya saa moja usiku, Kizza Besigye alirejeshwa kwenye gereza la After 7pm Luzira,” alisema Winnie.

Kulingana na Winnie, alipoondoka hospitalini saa kumi alasiri, alimwacha Besigye akiwa mnyonge na hakuweza kutembea ama kuzungumza. Alisema alimlisha kwa kuwa mikono yake haikuwa na nguvu.

Winnie alisema madaktari walikuwa na wasiwasi kuhusu hali yake na kwamba maafisa wa magereza walikuwa wameeleza awali kuwa gereza la Luzira halikuwa na uwezo wa kutoa huduma ya afya aliyohitaji.

Amesema uamuzi wa kumrudisha gerezani ulifuatia ziara ya Waziri wa Afya, Chris Baryomunsi, hospitalini.

Besigye,  amewahi kugombea urais wa Uganda mara nne bila mafanikio.

Share This Article