Baraza la Wazee kaunti ya Kakamega, limewaonya wanasiasa dhidi ya kuvuruga hafla za mazishi katika kaunti hiyo.
Kulingana na Baraza hilo, viongozi wa kisiasa ambao watahusishwa na ghasia katika hafla za mazishi watachukuliwa hatua kali, wakitaja hali za kusikitisha ambapo wahuni wametumika kuvuruga shughuli za umma.
Akizungumza Kakamega mjini, mwenyekiti wa Baraza hilo Elly Simwa, alitaja visa kadhaa ambapo wahuni wamezua ghasia na kusababisha majeraha na uharibifu mkubwa ma mali.
Aidha, mwenyekiti huyo aliwahimiza wanasiasa kuzingatia maadili na heshima, akisisitiza kuwa hafla za umma hasaa mazishi hazipaswi kugeuzwa kuwa majukwaa ya ghasia.
Wakati huo huo alitoa wito kwa viongozi kumpa fursa Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa kutekeleza majukumu yake na kutangamana na wakazi wa kaunti hiyo bila mwingilio wowowte.