Katika wa Afya ya umma Mary Muthoni,amefanya kikao na maafisa wa wizara ya afya wanaohudumu katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa KJIA, kutathmini kujiandaa kwao kukabiliana na visa vya ugonjwa wa Ebola.
Walifiakana kuongeza juhudi za kuwachunguza abiria wanaoingia humu nchini ili kubaini maambukizi ya mapema, hususan katika milango ya wageni wanaowasili kutoka mataifa yenye visa vingi vya maambukizi ya Ebola.
Wizara ya afya imewataka Wakenya kuwa watulivu na kuepuka habari za kupotosha.
Wakati uo huo Muthoni alizindua rasmi mpango wa kutoa vifaa vya kimatatibu vya kukabiliana na maambukizi ya Ebola katika maeneo mbalimbali humu nchini.

Vifaa hivyo vya matibabu ambavyo ni msaada kutoka kwa shirika la Amref kwa ushirikiano na serikali ya Marekani pamoja na UNICEF vitasaidia katika kukabiliana na Ebola.
Kenya tayari imeripoti visa viwili vya Ebola kutoka kwa mwanaume aliyefariki baada ya kuwasili nchini kutoka DR Congo huku jamaa wake wa karibu aliey na umri wa miaka 39 pia akipatikana na maambukizi ya virusi hivyo siku ya Jumatano baada ya kujitenga katika Karantini.