Ruto aendeleza ziara ya ukaguzi miradi ya maendeleo bonde la ufa

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto siku ya Alhamisi ameendeleza ziara yake kimaendeleo katika kaunti za bonde la Ufa.

Akiwa kaunti ya Elgeyo Marakwet,Ruto alikagua ujenzi wa soko la kisasa la Chepkorio AHP, na kufungua mradi wa uunganishaji umeme wa Last Mile eneo la Chepkorio na uzinduzi wa ujenzi wa barabara ya Chepkorio-Kipsaina kwa gharama ya shilingi bilioni 1.8 .

Rais aidha,amekagua ujenzi wa soko la kisasa la Chepkorio litakalomudu wafanyabisahara 200 huku likigharimu shilingi milioni 250 na ujenzi wa chuo cha kutoa mafunzo ya matibabu nchini KMTC.
Baadaye Rais likagua ujenzi wa uwanja wa michezo wa Kamariny mjini Iten na ujenzi wa nyumba 380 za gharama nafuu  katika eneo la Chepkorio eneo bunge la Keiyo  Kusini.
Katika kaunti  Baringo  Rais Ruto amezindua ujenzi wa barabara ya kilomita  70 ya Timboroa-Seguton-Arama-Moringwo na ile ya  Poror-Magrib-Sirwa-Lawina-Ochii eneo bunge la  Eldama Ravine kwa gharama ya shilingi bilioni 4.2.
Aidha,Ruto alizindua mradi wa uunganshaji umeme wa shilingi milioni 78.9 unaotarajiwa kuunganisha nyumba 343 na akafungua afisi za Huduma centre kaunti ya baringo ili kuleta huduma za serikali karibu na wananchi.
Share This Article