Mgonjwa aliyeshukiwa kuwa na maambukizi ya ugonjwa wa Ebola amepatikana kuwa hana virusi vya Bundibugyo, kulingana na uchunguzi wa maabara.
Matokeo hayo yanaondoa hofu iliyokuwa imezagaa kuhusu uwezekano wa Kenya kunakili kisa cha pili cha Ebola kufuatia kifo cha mgonjwa wa kwanza aliyewasili mapema wiki hii kutoka nchini DRC.
Mgonjwa huyo ambaye ni mwanamume wa umri wa miaka 20, alikuwa ametengwa katika hospitali ya kaunti ya Wajir.
Hii ni baada ya kubainika kuwa alikuwa amesafiri kutoka DRC kupitia Uganda kabla ya kuingia Kenya.
Kenya ni taifa la nne kuripoti kisa cha ugonjwa wa Ebola huku DRC ikiongoza kwa kunakili idadi ya watu 4,205 walioambukizwa kati ya watu 8,700 waliofanyiwa vipimo.