Nairobi kukabiliwa na uhaba wa maji Ijumaa na Jumamosi

Nairobi Water imewataka wanaoishi katika mitaa hiyo kuhifadhi maji ya kutosha kwa matumizi hadi huduma za kawaida za usambazaji zitakaporejea.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wakazi wa maeneo kadhaa ya kaunti ya Nairobi watakabiliwa na uhaba wa maji baina ya leoi Ijumaa Septemba 11 na Jumamosi tarehe 12, kutokana na ukarabati unaotarajiwa kufanywa na kampuni ya usambazaji maji ya Nairobi.

Maeneo yatakayoathiriwa na uhaba huo ni pamoja na;Westlands,Kileleshwa,Dagoretti,Upper Hill,Kawangware na katika makao makuu ya Chuo Kikuu cha Nairobi.

Nairobi Water imewataka wanaoishi katika mitaa hiyo kuhifadhi maji ya kutosha kwa matumizi hadi huduma za kawaida za usambazaji zitakaporejea.

Ukarabati huo wa dharura wa mabomba unatarajiwa kuchukua muda wa siku mbili.

Share This Article