Maonyesho ya kimataifa ya Kilimo na biashara ya Nairobi yameingia siku ya tano leo Ijumaa katika uwanja wa Jamhuri, kaunti ya Nairobi.
Maonyesho hayo yalifunguliwa rasmi Alhamisi na Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe.
Wakulima, wafanyabiashara na waonyesha bidhaa hutumia maonyesho hayo kutangaza na kuuza bidhaa.
Aidha, wanafunzi walimiminika kwa wingi kujionea bidhaa, mifugo na mimea inayoonyeshwa.
Tiketi za maonyesho hayo yatakayokamilika Jumapili hii, Oktoba 4 zinauzwa kwa shilingi 300 kwa watoto na shilingi 350 kwa watu wazima.