Idadi ya walioambukizwa Ebola DRC yafika 3,200

Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa, ugonjwa huo umeenea katika majimbo matano, yakiwemo mawili mapya ambayo yamenakili visa vya ugonjwa huo hivi majuzi.

Tom Mathinji
1 Min Read
Idadi ya maambukizi ya Ebola DRC yafika watu 3,200.

Mamlaka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), imesema kuwa idadi ya watu walioambukizwa ugonjwa wa Ebola imefika 3,200, asilimia 90 ya walioambukizwa wakiwa mkoa wa Ituri.

Kwenye takwimu hiyo iliyotolewa siku ya Jumapili, watu 1,405 wamefariki hadi sasa kutokana na maambukizi ya ugonjwa huo, huku maambukizi hayo yakiongezeka kwa visa 1,000 katika muda wa siku 10.

Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa, ugonjwa huo umeenea katika majimbo matano, yakiwemo mawili mapya ambayo yamenakili visa vya ugonjwa huo hivi majuzi.

Maafisa nchini DRC wamesema kuboreshwa kwa uchunguzi na upimaji, kumesababisha kugunduliwa kwa maambukizi mengi zaidi.

Ebola huenea kwa kugusa majimaji ya mwili wa mtu aliyeambukizwa, na husababisha homa kali inayoweza kuambatana na kutokwa damu.

Katika kipindi cha miaka 50 iliyopita ugonjwa huu umeua zaidi ya watu 15,000 barani Afrika.

TAGGED:
Share This Article