Gari la kifahari la shilingi milioni 77 la Spika wa Uganda lakamatwa

Gari hilo jipya aina ya Rolls-Royce Cunnin SUV lilitengenezwa mwaka 2025, huku Spika Among, akililipia ushuru wa shilingi bilioni moja za Uganda sawa na shilingi milioni 34.4 za Kenya pesa taslimu.

Dismas Otuke
1 Min Read

Maafisa wa polisi nchini Uganda wamelikamata gari la kifahari la Spika anayeondoka Anita Among la thamani ya shilingi milioni 77.6 za Kenya sawa na shilingi bilioni 3.4 za Uganda.

Gari hilo liliibua mjadala mkubwa nchini Uganda huku Rais Yoweri Museveni, akiamrisha kuchunguzwa kwa Among kwa madai ya ufisadi.

Polisi wamekuwa wakifanya msako nyumbani kwa Spika huyo tangu Ijumaa iliyopita kutafuta stakabadhi zinazoshukiwa kutumika kwa uporaji wa pesa za umma.

Gari hilo jipya aina ya Rolls-Royce Cunnin SUV, lilitengenezwa mwaka 2025, huku Spika Among, akililipia ushuru wa shilingi bilioni moja za Uganda sawa na shilingi milioni 34.4, za Kenya pesa taslimu.

Spika wa Uganda Anita Among

Mamlaka ya Uganda ilishangazwa ni vipi Among, alimiliki kiwango kikubwa hivyo cha pesa  za kulipia ushuru wa gari hilo.

Kutokana na shutuma kali na kusakamwa na serikali, Among amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha kuhifadhi kiti chake cha Spika wa bunge la Uganda.

Share This Article