Vituo vingi vya magari ya usafiri wa umma nchini vilisalia bila magari Jumatatu, katika maeneo mengi nchini Kenya, katika siku ya kwanza ya mgomo wa kitaifa wa wenye matatu kupinga kuongezwa kwa bei ya mafuta.
Kituo kikuu cha mabnasi kaunti ya Kisumu, hakikuwa na magari huku abiria wakitaabika ,sawia na vituo vya Nakuru,Eldoret,Naivasha ,Bomet na Kisii.
Vituo vichache vilivyokuwa na magari Jumatatu Alfajiri, vilishuhudia wasafiri wakilipishwa nauli mara dufu.
Jijini Nairobi hali ilikuwa ya mshikemshike polisi wakikimbizana na vijana waliojaribu kuziba barabara.