Watu wawili wameripotiwa kuaga dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati wa tetemeko kubwa la ardhi lilipotokea eneo la Guangxi, nchini China siku ya Jumatatu.
Tetemeko hilo la ukubwa wa 5.2, kwenye kipimo cha Richter limewalazimu zaidi ya watu 7,000 kutoroka makwao katika mji wa Liuzhou.
Nyumba 13 ziliporomoka katika mkasa huo wa mapema Jumatatu ambao ulivuruga usafiri.
Hata hivyo, reli na laini za mawasiliano hazikuathiriwa kutokana na tetemeko hilo.