Mourinho akubali kurejea Real Madrid

Mourinho akubali kurejea Real Madrid

Dismas Otuke
0 Min Read

Aliyekuwa Meneja wa Real Madrid, Jose Mourinho, amekubali kurejea kuwafunza miamba hao wa Uhispania,takriban miaka 11 tangu apigwe kalamu.

Yamkini Mourinho, ameafikiana na wasimazi wa Madrid, na anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili  mwezi ujao.

Madrid imefunga msimu wa mwaka 2025/2026 bila taji lolote.

Hadi uteuzi wake, Mourinho amekuwa meneja wa klabu ya nyumbani kwao Benfica, na ameingoza kumaliza ya tatu ligini.

Share This Article