Marefarii watatu wamefungiwa kusimamia mechi za Ligi Kuu Kenya na shirikisho la FKF kwa kukiuka sheria za usimamishi mechi.
Kamati ya usimamizi mechi za ligi Kuu iliafikia uamuzi huo baada ya kutazama kwa video za mechi zilizosimamiwa na waamuzi hao.
Marefarii hao walitoa adhabu ya marufuku ya mechi tatu kwa waamuzi hao baada ya kubaini kuwa walishindwa kudhibiti mechi .
Mmoja wa marefa hao ameshushwa ngazi na takuwa akisimamia mechi za ligi ya NSL, huku wengine wengine wawili wakifungiwa mechi tatu.
Aidha, marefa hao watatu watachunguzwa kwa karibu kabla ya kurejeshwa kusimamia mechi.