Visa viwili vipya vya Ebola vyanakiliwa Uganda

Tom Mathinji
1 Min Read
Visa viwili zaidi vya Ebola vyanakiliwa Uganda.

Uganda imetangaza kunakili visa viwili zaidi vya ugonjwa wa Ebola, na kufikisha 9 idadi jumla ya visa vya ugonjwa huo vilivyonakiliwa hadi sasa.

Kulingana na Wizara ya Afya ya Uganda, visa hivyo viwili vipya, vilinakiliwa katika Jiji Kuu la taifa hilo Kampala.

Taarifa hiyo inadokeza kuwa maambukizi hayo mapya yanaaminika kutoka kwa raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambao kwa sasa wako chini ya uangalizi wa madaktari.

Uganda tayari imefunga mpaka wake na DRC, kama hatua madhubuti ya kuzuia msambao wa ugonjwa huo wa Ebola ambao hadi sasa umesababisha vifo vya takriban zaidi ya watu 200, huku zaidi ya 1,000 wakiambukizwa.

Uganda pia imepiga marufuku mikusanyiko ya watu wengi na kuimarisha ukaguzi wa watu mipakani ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa huo wa Ebola.

Hadi kufikia sasa hakuna chanjo ya kutibu ugonjwa huo.

TAGGED:
Share This Article