Kenya na Marekani kuimarisha ushirikiano katika sekta ya usalama

Burns alisisitza kuwa hakuna taifa au shirika la kiusalama ambalo linaweza kutekeleza majukumu yake bila ushirikiano.

Tom Mathinji
1 Min Read
Kenya na Marekani kuimarisha ushirikiano wa kiusalama.

Kenya na Marekani zimeelezea kuimarisha ushirikiano wao katika masuala ya kiusalama.

Kwenye mkutano na Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja, Mjumbe wa Marekani hapa nchini Susan Burns, alisema mazungumzo hayo yaliangazia mifumo ya usalama mipakani, juhudi za kukabiliana na ugaidi, vita dhidi ya mihadarati na uhalifu unaopangwa wa kimataifa  ukiwemo ulanguzi wa fedha.

Burns alisisitza kuwa hakuna taifa au shirika la kiusalama ambalo linaweza kutekeleza majukumu yake bila ushirikiano, huku akimhakikishia Kanja ushirikiano ulioimarika zaidi.

Kwa upande wake, Inspekta jenerali Kanja alitambua ushirikiano thabiti unaoendelea kati ya nchi hizo mbili, huku akiishukuru Marekani kwa kuendeleza mafunzo ya  pamoja kwa manufaa ya pande mbili.

Huku akitaja changamoto zinazokabili sekta ya afya, Kanja alisema ipo haja ya ushirikiano wa kuimarisha ushirikiano wa kimkakati.

Aidha aliangazia miradi ya mafunzo ya pamoja inayoendelea, akisema ustawishaji wa utaaluma  ni muhimu katika kudumisha usalama na uimarishaji wa utoaji huduma.

Share This Article