Kaunti ya Kirinyaga imenakili kupungua kwa kiwango kikubwa, kufuatia kuzinduliwa kwa hospitali za kuwashughulikia watoto.
Huku Kenya inapojiunga na mataifa mengine kuadhimisha wiki ya kimataifa ya kunyonyesha watoto, serikali ya Kirinyaga imejizatiti kutekeleza mpango wa kuimarisha hospitali za kuwahudumia watoto, kama juhudi za kupunguza vifo vya watoto wanaozaliwa.
Mpango huo ulioanzishwa kufanikisha kuwanyonyesha watoto waliozaliwa Kwa muda wa miezi sita mfululizo, umesifiwa kwa kupunguza maafa hayo.
Vifo vya watoto wanaozaliwa katika kaunti hiyo vimepungua kutoka vifo 26 kati ya watoto 1,000 wanaozaliwa hadi vifo 10 kwa kila watoto 1,000 wanaozaliwa.
Mpango huo unajumuisha kuwa na sera ya kuwanyonyesha watoto wanaozaliwa, kujadili umuhimu wa kuwanyonyesha watoto kwa kina mama wajawazito na familia zao na mgusano wa moja kwa moja wa ngozi kati ya mtoto na mama.
Akizungumza kwenye maadhimisho hayo, Mkurugenzi wa Afya ya Umma Dk. Peter Irungu alisema maziwa ya mama ndio chanjo ya kwanza kwa mtoto, alisema hutekekeza umuhimu mkubwa kuimarisha Kinga ya mtoto na kumlinda dhidi ya magonjwa tangu alipozaliwa.
“Maziwa ya mama ndio chanjo ya kwanza kwa mtoto,” alisema Dkt. Irungu.