UNODC itaimarisha utekelezaji wa majukumu yake, asema Monica Juma

Aliyasema hayo alipokuwa akiadhimisha mwezi wa nne tangu alipoteuliwa kwenye afisi hiyo yenye makao yake nchini Austria.

Tom Mathinji
1 Min Read
Monica Juma - Mkurugenzi Mkuu wa afisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mihadarati na Uhalifu (UNODC).

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu Mihadarti na Uhalifu (UNODC) Monica Juma, amesema afisi yake inajizatiti kuimarisha utekelezaji wa majukumu yake.

Akizungumza leo Ijumaa katika mkutano na wafanyakazi wa UNODC Jijini Viena Austria, Juma alisema amefanikiwa kulainisha mikakati ya afisi hiyo katika kukabiliana na uhalifu wa kupangwa wa kimataifa, utumizi na ulanguzi wa mihadarati, ufisadi na ugaidi kupitia utumizi wa teknolojia.

Aliyasema hayo alipokuwa akiadhimisha mwezi wa nne tangu alipoteuliwa kwenye afisi hiyo yenye makao yake nchini Austria.

“Miezi minne afisini na sasa tumepata mwelekeo,” alisema Juma kupitia taarifa katika ukurasa wa X.

Alielezea umuhimu wa ushirikiano wa karibu na Austria, kuhakikisha malengo ya UNODC yanafanikiwa bila changamoto.

TAGGED:
Share This Article