Wizara ya Kilimo yaweka mikakati kukabiliana na wizi wa mifugo

Licha ya kukabiliana na wizi wa mifugo, ANITRAC pia itafanikisha kuwafuatilia mifugo, kuimarisha uchunguzi wa magonjwa na kuisaidia Kenya kutimiza matakwa ya soko la kimataifa kuhusu afya ya mifugo,

Tom Mathinji
1 Min Read
Mutahi Kagwe - Waziri wa Kilimo na Ustawi wa Mifugo.

Waziri wa Kilimo na Ustawi wa Mutahi Kagwe, amesema mifugo wote ni sharti wawe na vitambulisho kwenye masikio, huku serikali ikitumia teknolojia kukabiliana wizi wa mifugo.

Kagwe alidokeza kuwa kila ng’ombe atakuwa na kitambulisho cha manjano kwenye masikio almarufu ANITRAC, hatua itakayowezesha kuwafuatilia mifugo na kuzuia usafirishaji na uuzaji haramu wa mifugo.

“Kila ng’ombe atakuwa na ANITRAC ya manjano kwenye masikio. Ukipatikana na mifugo bila kitambulisho hicho, utafafanua kwa polisi. Yeyote atakayepatikana akiwa na mifugo waliokatwa masikio, atakamatwa na polisi,” alisema Waziri Kagwe.

Licha ya kukabiliana na wizi wa mifugo, ANITRAC pia itafanikisha kuwafuatilia mifugo, kuimarisha uchunguzi wa magonjwa na kuisaidia Kenya kutimiza matakwa ya soko la kimataifa kuhusu afya ya mifugo, usalama wa chakula na maeneo wanakotoka mifugo hao.

Kagwe alikuwa akizungumza alipofungua rasmi maonyesho ya kitaifa ya kilimo ya Nyeri 2026.

Share This Article