Serikali inajizatiti kumaliza uhaba wa maziwa unaoshuhudiwa nchini .
Katibu wa mifugo Jonathan Mueke alisema haya alipotoa mitambo 12 ya kuhifadhi maziwa kwa chama cha ushirika cha wakulima wa ng’ombe wa maziwa kaunti ya Murang’a.
Mitambo hiyo itawanufaisha wakulima wapatao 18,500 kupunguza hasara ya kuharibika kwa maziwa.
Aidha mitambo hiyo ina uwezo wa kukusanya lita 37,000 za maziwa kwa siku.
Mueke alivitaka vyama vya ushirika kuhakikisha wakulima wanapata faida kutokana na bei bora ya maziwa katika soko.