Mkenya Caroline Gitonga ameshinda nishani ya fedha katika siku ya kwanza ya mashindano ya Riadha duniani kwa mbio za barabara za kilomita 5 mjini Copen Hagen,Denmark.
Gitonga alisajili muda wa dakika 14 na sekunde 48 nyuma ya Mwethiopia ,Likina Abebew aliyenyakua dhahabu kwa dakika 14 na sekunde 41.
Rose Davies wa Australia alinyakua medali ya shaba huku Mkenya mwingine Caroline Nyaga, akiridhia nafasi ya 13.
Mashindano hayo yatakamilika Jumapili kwa mbio za nusu marathon;bingwa wa dunia wa mbio za nyika Agnes Jebet Ng’etich,Daisilah Jerono,Veronica Loleo na Lillian Kassait, wakitimka mbio za wanawake.
Mbio za wanaume za nusu marathoni zitawashirikisha Daniel Ebenyo ,Nicholas Kipkorir,Alex Matata na Gideon Rono.