Raia wa Tanzania amekamatwa baada ya uchunguzi wa polisi kumhusisha na mauaji ya mtoto mwenye umri wa miaka 11, Kisauni.
Mtoto huyo Glorious Kaiza Maore aliripotiwa kutoweka Machi 15, 2026, alipokosa kufika nyumbani kutoka kanisani.
Siku kadhaa baadaye katika eneo la Manyani, mwili wa mtoto huyo ulipatikana ukiwa ndani ya gunia na umefungwa kwa kamba.
Idara ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), ilisema baada ya mwili huo kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya mafunzo na rufaa ya Pwani, ilibainika kuwa alikuwa amebakwa kabla ya kunyongwa.
DCI ilisema kuwa maafisa wake kutoka kituo cha polisi cha Kisauni walianzisha uchunguzi mara moja, huku matokeo ya uchunguzi wao yakiwaelekeza kwa Anthony Juma, almaarufu Kipara, kama mshukiwa Mkuu
Hata hivyo mshukiwa huyo alikuwa ametoroka nyumbani kwake akiwa ameacha nguo ambazo zilikuwa zimechoma, ishara kwamba alitaka kuharibu ushahidi.
Mshukiwa huyo ambaye hufaya kazi ya kuzoa taka, alikamatwa na anazuiliwa kwenye korokoro za polisi akisubiri kufikishwa mahakamani Mei 4,2026.