Samia apaa kuelekea Urusi kwa mwaliko wa Putin

Suluhu ni Rais wa pili wa Tanzania kuzuruUrusi tangu Rais Mwanzilishi wa taifa hilo Hayati Julius Nyerere, alipoalikwa kuzuru nchi hiyo mwaka 1969.

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameondoka kuelekea nchini Urusi kwa ziara rasmi kufuatia mwaliko wa Rais Vladimir Putin.

Suluhu ni Rais wa pili wa Tanzania kuzuru Urusi tangu Rais Mwanzilishi wa taifa hilo Hayati Julius Nyerere, alipoalikwa kuzuru nchi hiyo mwaka 1969.

Ziara hiyo ni muhimu kwa utekelezaji wa ruwaza ya Tanzania ya mwaka 2050, inayolenga kujumuisha ushirikishwaji zaidi wa sekta ya kibinafsi.

Aidha, Rais Samia atashiriki kwenye kongamano la kimataifa la  uwekezaji na kutangaza Tanzania kama kitovu cha uwekezaji.

 

Share This Article