Wizara ya Afya imetangaza kisa cha tatu cha virusi vya ugongwa wa Ebola kutoka kwa mwanammke mmoja mwenye umri wa miaka 65.
Mwanamke huyo aliyepatikana anahusiana kwa karibu na mgonjwa wa kwanza wa Ebola aliyefariki pamoja na mgonjwa wa pili aliye kwenye karantini.
Mkurugenzi Mkuu wa matibabu Patrick Amoth, amesema kuwa vipimo vyote viwili kutoka kwa mwanamke huyo katika maabara ya KEMRI na kituo cha kitaifa ch serikali cha kubaini virusi, vilibaini kuwa ana virusi vya Bundibugyo.
Mwanamke huyo anapokea matibabu katika kituo cha magonjwa ya kuambukiza .
Hata hivyo Amoth amesema serikali haitaweka masharti ya usafairi wala kutangamana kwani hakuna kisa chochote kilichoripotiwa katika jamii.
Kulingana na Amoth watu 127 kati ya 130 waliotangamana na mgonjwa wa kwanza wa Ebola, aliyeaga dunia tayari wametambuliwa na wametengwa huku juhudi zikiendelea kuwatafuta watatu waliosalia.
Mwanaume aliyefariki kutokana na Ebola alikuwa amewasili nchini kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, mnamo Oktoba 6 mwaka huu.