Maafisa wawili wa polisi wakamatwa kwa madai ya kupokea hongo

Maafisa hao Senior Sergent  Robert Kibet Businei na konstebo Janet Rose Makena, walikamatwa kwenye msako uliotekelezwa na maafisa wa EACC.

Tom Mathinji
1 Min Read
Maafisa wawili wa Polisi wakamatwa kwa kuitisha na kupokea hongo.

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), imewakamata Maafisa wawili wa Polisi wa Trafiki kwa madai ya kuitisha na kupokea hongo kutoka kwa madereva kwenye barabara ya  Maua–Makutano kaunti ya Meru.

Maafisa hao Senior Sergent  Robert Kibet Businei na konstebo Janet Rose Makena, walikamatwa kwenye msako uliotekelezwa na maafisa wa EACC.

Wakati wa operesheni hiyo, maafisa wa EACC walipata shilingi 23,000 kutoka kwa washukiwa hao, na kunasa gari aina ya Toyota Fielder lenye nambari za usajili KDC 873T, linaloaminika lilikuwa linatumiwa na maafisa hao wa polisi.

Kupitia kwa ukurasa wa X, EACC ilisema washukiwa hao walipelekwa katika afisi za kanda hiyo Isiolo mjini, kuhijiwa na kuandikisha taarifa.

EACC ilielezea kujitolea kwake kukabiliana na ufisadi na kuhakikisha maafisa wa umma wanazingatia viwango vya juu vya maadili na uwajibikaji wanapotekeleza majukumu yao.

TAGGED:
Share This Article