Wagonjwa 5 wa Ebola wapona, waondoka hospitalini

Wagonjwa wawili walitibiwa katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta, KNH huku watatu wakitibiwa katika hospitali ya Nairobi Hospital. 

Martin Mwanje
1 Min Read
Maafisa wakikabiliana na ugonjwa wa Ebola DRC.

Wagonjwa , wote wanaume, walioambukizwa ugonjwa wa Ebola wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kuthibitishwa kupona ugonjwa huo. 

Wawili walitibiwa katika hospitali ya rufaa ya Kenyatta, KNH huku wawili wakitibiwa katika hospitali ya Nairobi Hospital.

Wote hao walithibitishwa kutoonyesha dalili baada ya kupokea matibabu na vipimo kuonyesha hawana tena maambukizi ya ugonjwa wa Ebola.

“Zaidi ya hayo, watu 46 waliotangamana na wagonjwa hao wamekamilisha kipindi chao cha ufuatiliaji na wako katika hali nzuri ya afya wameondolewa katika karantini na kujiunga tena na familia zao,” alisema Waziri wa Afya Aden Duale kwenye taarifa.

“Watu 52 waliosalia wanatarajiwa kuruhusiwa kuondoka karantini kufikia Novemba 11, 2026, baada ya kukamilisha kipindi cha siku 21 tangu kutangamana kwao.”

Idadi ya visa vya ugonjwa wa Ebola vilivyothibitishwa kufikia sasa nchini vinasalia kuwa 9 huku waliofariki kutokana na ugonjwa huo wakisalia kuwa watu wawili.

Duale akidokeza kuwa hakuna kisa chochote cha ugonjwa wa Ebola kimeripotiwa nchini tangu Oktoba 9 mwaka huu.

 

 

 

Share This Article