Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa leo Jumatano limechagua wanachama watano wapya wasio wa kudumu wa Baraza la Usalama kwa muhula wa 2027–2028.
Nchi ambazo zinajiunga na baraza hilo ni pamoja na Austria, Ureno, Zimbabwe, Trinidad na Tobago na Zimbwabwe.
Zimbabwe inachukua pahala pa Somalia, Trinidad na Tobago ikichukua nafasi ya Panama, nayo Ureno na Austria zikipokezana kijiti na Denmark na Greece ambazo zitahudumu hadi mwisho wa mwaka 2026.
Nchi hizi zilizochaguliwa zitahudumu kwa kipindi cha miaka miwili kuanzia tarehe 1 Januari 2027 hadi 31 Desemba 2028.
Uchaguzi wa wanachama wa Baraza la Usalama hufanyika kwa kura ya siri, na kila mgombea hutakiwa kupata theluthi mbili ya kura kutoka kwa nchi zote wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa.
Viti hugawiwa kulingana na makundi ya kijiografia ili kuhakikisha uwakilishi wa haki kutoka kila eneo.