Washukiwa wawili wa wizi wa Mifugo wamekamatwa huku mifugo waliobwa walipatikana katika kaunti ya Bungoma.
Operesheni ya pamoja ilitekelezwa baada ya wamiliki mifugo kuripoti kutoweka kwa mifugo 14 walipokuwa malishoni katika msitu wa Kaperua.
Baada ya operesheni hiyo, mifugo 12 walipatikana katika msitu wa Kipsigon, kaunti ndogo ya Kopsiro.
Wawili hao Kwa sasa wanazuiliwa, wakisubiri kufikishwa mahakamani.
Mipango inaendelea ya kuwatambua mifugo hao na kukabidhiwa wenyewe halali.
Huduma ya Taifa ya Polisi imeelezea kujitolea kwake kushirikiana na asasi zingine za usalama na wananchi kukabiliana na wizi wa mifugo.