Maafisa wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai DCI, wamemkamata mshukiwa wa ulaghai wa ardhi anayedaiwa kupokea shilingi 900,000 kwa njia ya udanganyifu.
Mshukiwa huyo Andrew Gachagua Njui, alikamatwa baada ya Polisi kupokea habari kutoka kwa mnunuzi aliyeshuku ununuzi wa ardhi katika eneo la Molo kaunti ya Nakuru.
Baada ya mnunuzi huyo kumlipa mshukiwa shilingi 900,000, baadaye aligundua ardhi hiyo haikuwa ya mshukiwa huyo lakini ilikuwa imesajiliwa kwa jina la mtu mwingine.
Mshukiwa huyo alitarajiwa kufika mahakamani Mei 26,2026 katika mahakama ya hakimu mwandamizi ya Molo, lakini hakufika swala lililosababisha mahakama kutoa ilani ya kukamatwa kwake.
Baada ya operesheni ya kina, mshukiwa huyo alikamatwa katika eneo la Othaya kaunti ya Nyeri na kuzuiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani.