Wanajeshi wanne wa Uganda wamewekwa rumande katika korokoro ya kijeshi ya Makindye jijini Kampala,Uganda, kwa kushukiwa kuhusika katika wizi wa mafuta ya gari.
Maafisa wa hao wakuu katika jeshi la Uganda UPDF wakiwemo Brigedia James Barigye mwenye umri wa miaka 60,Kanali David Kidega aliye na umri wa miaka 52,Meja Innocent kikongi mwenye umri wa miaka 41, na Kapteni Keneth Kinyera aliya na umri wa miaka 37, walifikishwa katika mahakama ya kijeshi ya Makindye siku ya Jumatatu kula viapo.
Wanajeshi hao wanashtakiwa kwa kuiba lita 270,000 za mafuta ya gari.
Wanne hao yakimini kati ya Julai mwaka 2022 na Disemba mwaka 2023, walipora mafuta hayo yaliyolenga kutumika kupasha moto zana za kijeshi na walikamatwa mwaka uliopita.
Maafisa hao walitiwa mbaroni mwaka jana kufuatia ripoti iliyothibitisha kupotea kwa mafuta na watasalia korokoroni hadi tarehe 29 mwezi ujao wakati wa kuskizwa kwa kesi hiyo.