Mahakama yafunga kesi ya Chemutai

Mumewe aliwasilisha kesi hiyo kupinga mipango ya mazishi na kutaka ajumuishwe na kutoa uamuzi wa mwisho, jambo ambalo faimilia ya marehemu ilipinga.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mahakama ya Milimani ilifunga kesi kuhusu utata wa mazishi ya aliyekuwa Msimamizi wa Data wa benki ya Kenya Commercial Rosemary Koech Kimwatu, baada ya mumewe kuondoa mashtaka aliyokuwa amewasilisha kupinga mazishi.

Kelvin Migwe Kimwatu aliondoa kesi hiyo baada ya kuthibitisha kuwa marehemu alikuwa tayari amezikwa.

Mumewe aliwasilisha kesi hiyo kupinga mipango ya mazishi na kutaka ajumuishwe na kutoa uamuzi wa mwisho, jambo ambalo faimilia ya marehemu ilipinga.

Ilimbidi Kimwatu aondoe kesi kufuatia kufahamu kuwa marehemu alikuwa tayari amezikwa usiku, kabla ya kesi hiyo kuanza na hakutaka mahakama itoe amri ya kufukuliwa kwa mwili wake.

Share This Article